QUEEN DARLEEN: NAMPENDA SANA ZARI!

MWANAHAWA Abdul ambaye wengi humfahamu kwa jina la Queen Darleen ni ‘first lady’ wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ili chini ya kaka yake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kwa sasa ana miaka 15 ndani ya Bongo Flava. Queen Darleen analia na skendo inayomtafuna kuwa yeye anajihusisha na mambo ya kisagaji.

Akizungumza ana kwa ana na Over Ze Wekeend, Queen Darleen ambaye pia ni dada wa Diamond anafafanua kuhusu jambo hilo na mambo mengine mengi;

Over ze Weekend: Najua umeanza muziki muda mrefu sanam je, ni changamoto gani umekutana nayo kama mwanamuziki wa kike?

Queen Darleen: Unajua mimi sikupata changamoto kubwa sana kupenya kwenye muziki kwa sababu nilikuwa nimeshikwa mkono na kaka Dully (Dully Sykes).

Labda changamoto ya kutongozwa na maprodyuza tu, lakini si vinginevyo.

Over Ze Wekeend: Vipi hiyo ya kutongozwa na maprodyuza, je, ulipona kweli kuingia kwenye laini?

Queen Darleen: Unajua kwanza mimi ilikuwa mtu akinitongoza tu, lazima nimwambie Dully au mjomba wangu, Tudo.

Over Ze Weekend: Unasema kuwa waliokushika mkono mmojawapo ni Dully, vipi kuhusu Ali Kiba maana wengi walijua ni ndugu yako?

Over Ze Weekend: Yaani Kiba tuliimba naye wimbo mmoja tu kwa sababu wote tulikuwa chini ya Lebo ya G- Lover na si vinginevyo. Pia mara nyingi sipendi kumuongelea kwa sababu nikiongea inakuwa tofauti.

Over Ze Weekend: Mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii umekuwa ukirushiwa vijembe mbalimbali kutokana na uvaaji wako, hilo unalizungumziaje?

Queen Darleen: Unajua mimi hayo ndiyo mavazi yangu niliyoyazoea siku zote maana hadi wengine wanasema mimi msagaji, lakini mimi kwenye mavazi siko kihivyo?

Over Ze Weekend: Kwani ulishawahi kukumbwa na skendo hiyo ya usagaji?

Queen Darleen: Sana tu, hadi sasa hivi ipo hadi huwa najiuliza ni nani niliyewahi kumsaga? Basi kama yupo ajitokeze, akiri jambo hilo ili ijulikane.

Over Ze Weekend: Kuna kipindi ulisema kuwa hutongozwi, je, ni kwa nini?

Queen Darleen: (kicheko) unajua mimi kwa kweli hata nikijichunguza waliowahi kunivua nguo, hawafiki hata watano ndiyo maana nilisema hivyo.

Over Ze Weekend: Watu wengi wanajua wewe huna mtoto, lakini pia walishangaa kusikia ukisema wewe bado una usichana wako, hili likoje?

Queen Darleen: Ukweli ni kwamba mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Anaitwa Rooney, kuhusu kuwa na usichana, huo ni utani tu!

Over Ze Wekeend: Mara nyingi umekuwa hupendi kabisa kuweka uhusiano wako wa kimapenzi hadharani, je, ni kwa nini?

Queen Darleen: Sipendi tu kwa sababu niliye naye tuna mwaka sasa, lakini mtu hawezi kujua. Pia ninapenda kuwa na uhusiano na mtu wa kawaida kabisa.

Over Ze Weekend: Hivi karibuni baba yako Mzee Abdul Jumaa alitoa kauli kali kuwa hata akifa usifike kwenye msiba wake, akidai umemtukana, vipi kuhusu hilo?

Queen Darleen: Kuhusu hilo ni mambo ya kifamilia zaidi na pia yule ni baba yangu, ataendelea tu kuwa baba yangu daima.

Over Ze Weekend: Ukija kwenye upande wa mawifi (wachumba wa Diamond), watu wanasema huwa hutabiriki kabisa. Je, wewe upo upande gani maana kwa Zari ulikuwepo, kwa Wema na kwa Penny pia ulikuwepo, vipi kuhusu hilo?

Queen Darleen: Kwanza kabisa watu wajue mimi ninampenda sana Zari, tena sana, lakini huko nyuma nilimpenda Wema kwa sababu alikuwa ndiye wifi kwa kipindi hicho. Penny ni rafiki yangu hadi sasa.

Over Ze Weekend: Mbona hujamtaja wifi yako mmoja ambaye ni Hamisa Mobeto aliyewapa zawadi ya mtoto?

Queen Darleen: Ninachojua Hamisa ni mama Abdul, lakini sina mazoea naye sana. Tulikuwa tukionana juu kwa juu kwenye sherehe mbalimbali. Hata hivyo, Diamond hafuatilii kabisa mambo yangu ya uhusiano, sasa kwa nini mimi nimfuatilie?

Over ze Wekeend: Asante Queen Darleen kwa kwa ushirikiano wako.

Queen Darleen: Karibu tena na tena.

 

IMELDA MTEMA

Toa comment