Queen Darleen: Sitongozwi, natongoza

mwana-dada-queen-darleen-katika-pozi Na Imelda Mtema | Gazeti la Risasi Jumamosi Toleo la Jan 14, 2017

MWANAMUZIKI ambaye ni memba wa Kundi la WCB, Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’ aliye  pia dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kuwa katika mapenzi kitu ambacho hakipendi ni kutongozwa na mwanaume hivyo huwa anapenda kutongoza.

queen-darleenAkistorisha na Mikito Nusunusu Darleen, alisema kitendo cha yeye kumtongoza mwanaume anaamini kwamba anakuwa  amempenda kutoka ndani ya moyo wake lakini akitongozwa wakati mwingine wanaume wanakuwa ni waongo hawana nia ya dhati.

“Katika maisha yangu yote huwa sipendi kutongozwa napenda nitongoze kwa sababu naamini nikifanya hivyo nakuwa nimempenda mwanaume kweli kwani watongozaji wengi ni waongo na ninajijua kabisa  kwamba sina bahati kwenye mapenzi,” alisema.

Toa comment