The House of Favourite Newspapers

R Kelly Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa Kosa la Unyanyasaji wa Kingono

0

 

Msanii R Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela

MSANII maarufu wa R&B wa nchini Marekani Robert Kelly (55) maarufu kama R Kelly amehukumiwa jela kifungo cha miaka 30 kutokana na kukutwa na makosa ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na Watoto wadogo.

 

Kuelekea hukumu yake idadi ya wanawake walipaza sauti wakimzomea na kumtupia maneno R Kelly ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akishutumiwa kwa kujihusisha na matendo ya unyanyasaji wa kingono.

 

Tayari wakili wake amebainisha kuwa yeye na mteja wake watakata rufaa kupinga uamuzi huo uliotolewa na Jaji ambaye alibainisha kuwa R Kelly alikuwa na mtazamo tofauti wa kibinadamu dhidi ya wanawake.

 

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Angela alimuongelea R Kelly kuwa ni mtu ambaye aliishi Maisha ya kinyonge na kidhaifu.

“Nilihisi bora ningefariki tu kutokana na namna alivyonifanya nijisikie. Alisema Angela.

R Kelly akiwa Mahakamani wakati wa hukumu yake

Akiwa amevaa vazi la jela Pamoja na miwani myeusi Kelly aligoma kabisa kuongelea chochote mara baada ya hukumu kuwa imetolewa.

 

Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani Ann Donnelly amesema nyota huyo alitumia ngono kama chombo cha kuwanyanyasa wanawake na kuwalazimisha kufanya vitendo kinyume na matakwa yao huku akiwaambukiza had baadhi ya magonjwa ya zinaa.

 

“Uliwafundisha kuwa mapenzi ni vurugu na utumwa.” Alisema Jaji.

 

Katika hukumu hiyo kulikuwa na mvutano wa kisheria ambapo Mwanasheria wa Serikali aliomba R-Kelly afungwe zaidi ya miaka 25 kutokana na uzito wa kosa lake na nia ya kutaka kukomesha kabisa vitendo vya namna hiyo katika jamii huku Wakili wa R Kelly yeye akiiomba Mahakama imfungwe mteja wake kifungo cha miaka 10 ambacho ndiyo kiwango cha chini kabisa kisheria kwa mtu mwenye makosa ya aina hiyo.

Leave A Reply