The House of Favourite Newspapers

R.O.M.A, Isha, Snura ndani ya Dar Live kesho

0

romaMKALI wa miondoko ya Hip Hop Bongo, R.O.M.A Mkatoliki, mkali wa Taarab, Isha Mashauzi, mkali wa miondoko ya Mduara, Snura na wengine kibao kesho wanatarajiwa kutikisa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kwa kutoa bonge la shoo la kimataifa.

Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliitonya safu hii kuwa shoo hiyo itatambulika kama Usiku wa Nani Mkali. “Burudani itafunguliwa rasmi saa mbili ya usiku ambapo wakali wanaokimbiza kunako Muziki wa Singeli, Man Fongo na Shoro Mwamba watalishambulia jukwaa kwa kutoa nyimbo zao zote kali kuanzia Hauna, Hainaga Ushemeji na Sembe Tembele,” alisema Mbizo.

Mbizo aliongeza kuwa, R.O.M.A usiku huo ataisimamisha Dar Live kwa kupiga nyimbo zake zote kali kuanzia Mathematics, 2030 hadi Mtoto wa Kigogo. “Kwa wale wa Mduara tutakuwa naye Snura ambaye atakata nyonga na kupiga nyimbo zake nyingi kama Nimevurugwa, Majanga na nyinginezo.”

Mbizo alimaliza kwa kusema kuwa ili kuweka mzani wa burudani sawa, Dar Live itawadondosha pia wakali waMuziki wa Taarab, Mashauzi Classic wakiongozwa na Isha Mashauzi ambao watatoa burudani mwanzo mwisho.

“Mashauzi Classic itafunika na nyimbo zao zote kali kuanzia Mapenzi Hayana Dhamana, Mapenzi Yamenivuruga, Nimpe Nani na nyingine nyingi,” alisema Mbizo. Burudani hiyo itakayokwenda kwa kiingilio cha 8,000 tu getini, imedhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya

Leave A Reply