Raha Nazozipata Ndani ya Ndoa: MASELE

masele-chapombe-8Muigizaji wa vichekesho, Sipian Masele ‘Masele Chapombe’ ameyafungukia maisha yake ya ndoa tangu alipoamua kuvuta jiko ndani siku chache zilizopita kwa kumuoa muigizaji mwenzake, Specious kwa kusema kuwa anajuta kuchelewa kuoa.masele-chapombe-5

Akipiga stori na Global TV  Online leo, Masele  Chapombe amekuwa akijuta kuchelewa kuoa kwanimaisha ya ndoa ni mazuri kwa kuwa ni kitu alichokihitaji kwa muda mrefu na amekuwa haamini kama maisha ya ndoa yalikuwa matamu kiasi kwamba yamemfanya kujiona mwanaume mwenye bahati mno.

masele-chapombe-1“Maisha ya ndoa naona ni maisha mazuri,kwani ni maisha ya ukweli na uwazi. Miaka inaenda kusema nitafanya kesho sio sawa kabisa. Leo hii, ninajiona kuwa mwanaume mwenye bahati kuingia kwenye ndoa na kumpata mwanaume sahihi,” alisema Masele.

masele-chapombe-2

Aidha Masele aliambatana na mkewe, Specious nakueleza jinsi alivyouchukia ubachela hukuakiwataka vijana wenye umri unaostahili kuoa na wafanye hivyo kwani maisha ya ubachela hayakubaliki katika jamii. masele-chapombe-3

“Ubachela haufai. Wengine wanaogopa kuingia kwenye ndoa kwa kuwa wanaogopa changamoto. Ni kweli, kwenye maisha ya ndoa kuna changamoto lakini unatakiwa kupambana kwani hakuna kitu kizuri kiinachokosa changamoto,” alisema Masele. masele-chapombe-4Mbali na kuelezea maisha yake ya ndoa pia Masele alifunguka sababu iliyomfanya kuangua kilio siku ya harusi ambapo aliweka wazi kuwa kitendo cha rafiki yake, mchekeshaji mwenzake, Mkwere kukumbushia maisha ya nyuma, jinsi walivyosota kilikuwa kitu kilichomuumiza mno.  masele-chapombe-6

“Mpaka unaona nipo hivi, jua nimepitia mengi. Niliumia, nilikatishwa tamaa lakini nilipambana. Yote hiyo kwa sababu nilikuwa natafuta nikiwa na wenzake akiwemo Mkwere. Sasa kitendo cha kunikumbusha yale yaliyopita, niliumia lakini baadaye nikafarijika kila nilipojiona hapa niliposimama leo hii,” alisema Masele. masele-chapombe-7  masele-chapombe-9 masele-chapombe-10 masele-chapombe-11

Salum Milongo/GPL

Wiki Moja Baada ya Ndoa, Masele Chapombe Amtongoza Upya Mke Wake


Toa comment