Rais Apandisha cheo Kamishna kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna wa Magereza, CP Jeremiah Katungu kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) na kumteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, Blozi Dk. Moses Kusiluka, Katungu anachukua nafasi ya CGP, Mzee Ramadhan Nyamka ambaye amestaafu.