Rais Ashambuliwa kwa Kisu Msikitini

Rais wa Mali, Kanali Assimi Goïta yuko salama baada ya mshambuliaji aliyekuwa amejihami kwa kisu kumshambulia katika msikiti wa Bamako-Grande Mosque uliopo katika mji mkuu, Bamako ambako alikuwa amejiunga na waumini kwa ajili ya ibada ya Idd ul-Adha.

 

Taarifa ya ofisi ya rais imesema kuwa alishambuliwa na wanaume wawili, lakini ni mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu alikamatwa mara moja na rais aliondoshwa msikitini kwa gari mara moja hadi katika kambi za jeshi zilizopo nje ya jiji.

 

Waziri amelielezea shambulio hilo kama jaribio dhidi ya maisha ya rais. Umati mkubwa ulikuwa umekusanyika katia msikiti kwa ajili ya sala, ya Idd ya kuchinja kafala. Wengi waliisali kwenye viwanja vya msikitiImage caption: Wengi waliisali kwenye viwanja vya msikiti. Kondoo alitolewa kafara na Imam mwisho wa sala.

Shambulio linatia hofu kwa nchi inayokabiliwa na changamoto za kiusalama, ikiwa ni pamoja na uasi wa makundi ya jihad yanayofanya mashambulio ya mara kwa mara ya makundi yenye uhusiano naal-Qaeda na Islamic State.

 

Kanali Goïta ni mtu mwenye utata – kwa kufanya mapinduzi mawili ya kijeshi chini ya mwaka mmoja. Alijitangaza kama rais mwezi Mei baada ya kuiondoa mamlakani serikali iliyokuwa imewekwa baada ya kuongoza mapinduzi dhidi ya rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka jana. Aliahidi kuirejesha nchi katika utawala kamili wa kiraia mapema mwaka ujao.


Toa comment