The House of Favourite Newspapers

Rais Azuiwa Kushiriki Uchaguzi

0

RAIS wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amezuiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wa tume ya uchaguzi.

 

Wakili wake, Claude Mentenon, amelimbia shirika la habari la AFP kuwa kuna matatizo mengine zaidi ya kisheria ndani ya Ivory coast dhidi yake. Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilimuondoa katika orodha ya wagombea kwa sababu alipatikana na hatia ya uhalifu.

 

Rais wa tume ya uchaguzi , Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, alisema mwezi Agosti kwamba yeyote anayepatikana na hatia ya uhalifu ataondolewa kwenye orodha ya wagombea. Alitoa tangazo hilo wakati alipokuwa akitangaza orodha mpya ya wagombea.

 

Wagombea wanne akiwemo kiongozi wa zamani wa waasi, Guillaume Soro, waliondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais. Gbagbo aliondolewa mashitaka mwezi Januari 2019 baada ya kushtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu ambao ulihusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Leave A Reply