The House of Favourite Newspapers

Rais Barcelona Abwaga Manyanga

0

 

                                     Rais wa Barcelona aliyejiuzulu. Josep Maria Bartomeu.

KLABU  ya Barcelona imetangaza rasmi aliyekuwa Rais wao, Josep Maria Bartomeu, amejiuzulu nafasi hiyo pamoja na bodi yote ya wakurugenzi.

 

Bartomeu, 57, amekuwa Rais wa Barcelona tangu mwaka 2014, lakini homa  ya kuachia kiti hicho iliongezeka majira ya kiangazi mwaka huu baada nyota wa timu hiyo, Lionel Messi, na wachezaji wengine wa Barcelona kukosoa hadharani  uongozi wake hasa klabu hiyo ilivyokuwa inafanya sajili zake.

 

Uchaguzi utapangwa ndani ya siku 90 zijazo ili kuziba nafasi ya rais huyo.  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kupoteza mechi ya ligi   nyumbani  kwenye uwanja wa Nou Camp dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Real Madrid, kwa kipigo cha magoli 3-1.

Leave A Reply