The House of Favourite Newspapers

Rais Biden Atangaza Ongezeko la Ushuru kwa Magari ya Umeme ya China

0

Katika juhudi za kufufua viwanda vya ndani, Rais Joe Biden alitangaza Jumanne kwamba anaweka ongezeko kubwa la ushuru kwa magari ya umeme ya China na ushuru mpya kwenye vifaa vya kompyuta, vifaa vya nishati ya jua na betri za lithiamu-ion.

“Hatutairuhusu China kufunika soko letu na kufanya kuwa vigumu kwa wazalishaji wa magari ya Marekani kushindana kwa haki”, Biden alisema. “Nitafanya hivyo kwa kufuata sheria za kimataifa za biashara”.

Ushuru kwenye magari ya umeme ya China, au EVs, utaongezeka mara nne kwa kiwango cha asilimia 100. Uagizaji wa vifaa vya nishati ya jua na vifaa vidogo au semiconductor kutoka China vitatozwa ushuru wa asilimia 50, mara mbili ya kiwango cha sasa.

Kiwango cha uagizaji aina fulani ya chuma na bati, kitaongezeka hadi asilimia 25, mara tatu zaidi ya kiwango cha sasa. Ongezeko hilo la ushuru litafikia dola bilioni 18 katika bidhaa za China. Ushuru kwenye EVs, chuma na bati, pamoja na vifaa vya nishati ya jua utaanza kutumika mwaka huu, na mwaka ujao kwa vifaa vya ndani vya kompyuta.

 

Leave A Reply