The House of Favourite Newspapers

Rais Clinton Alazwa Hospitalini

0

RAIS wa zamani wa Marekani Bill Clinton (75) amepelekwa  kwenye kwenye Kituo cha Afya cha UC Irvine, California kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua.

 

Msemaji wake, Angel Ureña amesema kuwa Clinton anaendelea vizuri lakini bado halijawekwa wazi ugonjwa unaomsumbua licha kwamba inafahamika kuwa Clinton amekuwa na historia ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

 

Katika taarifa ya daktari anayemtibu anasema kuwa amempatia dawa za antibiotiki ili iweze kumsaidia. Daktari huyo aliongeza kuwa Clinton alibaki hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Madaktari wa UC Irvine wameanza mchakato wa kuwasiliana na timu ya matabibu wa Clinton huko New York, pamoja na daktari wake wa moyo.

 

Clinton amedumu kama Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1993 mpaka 2001. Lakini alipigiwa kura ya kutokuwa na imani nae mwaka 1998 baada ya kudanganya kuhusu uchunguzi uliofanyika juu ya kuhusishwa kutoka kimahusiano na msaidizi wake wa Ikulu, Monica Lewinsky.

 

Mwaka 2004, Clinton alifanyiwa upasuaji mara nne na miaka kumi baada ya kulalamika kwa maumivu ya kifua. Muda mfupi baada ya upasuaji wa pili, Clinton alikuwa anajulikana kwa kupenda vyakula vyenye mafuta vilivyomsababishia matatizo ya mshipa ya moyo.

 

Leave A Reply