The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais Dk. Hussein Mwinyi Akutana na Uongozi wa Nmb Ikulu Zanzibar

0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.Wengine ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kati), Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa, Alfred Shao na Mkuu wa Biashara Zanzibar wa Benki ya NMB, Abdalla Duchi.
Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, alipokuwa akielezea namna Benki ya NMB imejipanga  kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukuza uchumi na kuisaidia jamii.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkabidhi Dk. Hussein Ali Mwinyi  kadi ya yake ya NMB Mastacard World Debit.
…Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na kadi ya yake ya NMB Mastacard World Debit.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na uongozi wa Benki ya NMB Ikulu Jijini Zanzibar na kueleza kuwa yupo tayari kushirikiana na Benki hiyo kwa ajili ya kuimarisha uchumi pamoja na huduma za kijamii Zanzibar.

Rais Dk. Hussein amesema kuwa Benki ya NMB imepata mafanikio makubwa hivyo, Serikali anayoiongoza iko tayari kushirikiana na NMB katika kuimarisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Leave A Reply