The House of Favourite Newspapers

Rais Dk. Mwinyi Ahitimisha Ziara Yake Nchini Qatar, Azungumza na Diaspora

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amehitimisha ziara yake ya siku nne Doha, Qatar, kwa kuzungumza na baadhi ya Watanzania wanaoishi Qatar, maarufu kama wana-diaspora. Ziara yake ilijumuisha mazungumzo na viongozi wa Qatar, kusaini makubaliano muhimu, kuhudhuria Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi.

Katika mkutano huo Dk. Mwinyi alijibu hoja mbalimbali zilizoulizwa na wana-diaspora hao.

Baadhi ya hoja zilizotaka ufafanuzi ni sera ya uchumi wa Buluu, Wanafunzi kupatiwa nafasi kusoma Qatar, Uraia kwa watoto wanaozaliwa nje ya nchi na wazazi wawili Watanzania na pia suala la kodi wanazotozwa kwa biashara zao zilizopo Tanzania.

Dk Mwinyi alizitolea ufafanuzi hoja hizo huku nyingine zikijibiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk, Balozi Mahadhi, Balozi wa Tanzania nchini Qatar na pia Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Bw. Shariff A Shariff na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gelead Teri.

Dk. Mwinyi aliwasili Doha tarehe 21 Mei 2023 Jumapili usiku akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa tatu wa Jukwaa la Uchumi Qatar.

📆 24 Mei 2023

📍Doha, Qatar

Leave A Reply