The House of Favourite Newspapers

Rais Dkt. Samia ni Shupavu na Mwenye Maono

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Christina Mndeme amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi shupavu na mwenye maono ya kuongoza nchi.
Amesema hayo wakati Clouds TV  kwa kupitia Kipindi chake cha Sentro Bash la Bimdash wameungana na watanzania wengine katika kusherehekea kumbukizi ya tarehe ya kuzaliwa kwa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  aliyetimiza umri wa miaka 65 jana tarehe 27 Januari.
Mndeme amesema anamuombea Mheshimiwa Rais Dkt Samia kwa Mwenyeezi Mungu  ampe uhai na hekima zaidi ili aendelee kuiongoza nchi ya Tanzani huku amewataka watanzania kuendelea kumshkuru Mungu kwa kuwa kuwa na Kiongozi msikivu Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mwanamuziki mkongwe  wa muziki wa taarab nchini pia ni Malkia wa Mipasho  Afrika Mashariki Bi Khadija Omar Kopa  alitoa burudani na kuimba wimbo maalumu wenye mahadhi ya taarab.
“Rais Dkt.Samia mimi ni nduguangu namuombea mwenyeezi Mungu amzidishie nguvu na ari ya kuliongoza taifa  na kumzidishia umahiri wake katika kulitumikia taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema Bi Khadija.
Kopa ameongeza kwa kusema kuwa Dkt. Samia ameingia katika kipindi kigumu cha uongozi lakini hivi sasa kila Mtanzania anakula mema ya nchi katika nyanja mbalimbali kama wasanii ,wanamichezo amekuza michezo ikiwamo soka ambako amekua akitoa hamasa ya goli la mama bila kuwasa mchezo wa masumbwi” amesema Kopa.
Kopa ameongeza kwa kusema kuwa anamuombea kwa Mungu  Rais Dkt.Samia  aendelee kuiongoza nchi kwa amani na kusema mama ulipo tupo na huu ndiyo mwanzo wa ushindi.
Msanii mwingine ambaye ametumbuiza ni Barnaba Classic ambaye amesema anamshukuru sana Mhe.Rais Mama Dkt.Samia kwa sababu anawapenda sana wasanii huku akijinadi kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii ambao wanapata nafasi za kutoa burudani kwenye hafla nyingi za Serikali na hasa Ikulu.