The House of Favourite Newspapers

Rais Dkt. Magufuli Asaini Misamaha Ya Wafungwa 63

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini Nyaraka zenye majina ya Wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Familia ya Nguza Viking (Babu Seya), na Johnson Nguza waliopata msahama wa Rais, katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiyahakiki kwa kuyasoma majina ya Wafungwa 63 waliopata msahama wa Rais kabla ya kutia saini Nyaraka hizo za Msamaha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutia saini majina ya wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Wafungwa Nguza Viking(Babu Seya), na Johnson Nguza waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Rais John Magufuli amesaini nyaraka za wafungwa 63 ambapo wafungwa 61 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa na wawili kifungo cha maisha.  Nyaraka hizo alizisaini mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa huko Dodoma.

Katika msamaha huo wamo wanamuziki wawili, Nguza Viking na Papii Kocha waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha na ambao tayari waliachiwa jana.

 

 

 

Comments are closed.