Rais Dkt.Samia ateua Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kabla ya uteuzi huu Kaji alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.