Rais Dkt. Samia Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Msikiti wa Al Ghath Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti wa Al Ghaith uliopo eneo la Kilakala Flats, Mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba, 2024. Rais Dkt. Samia amewasisitiza waislamu kujenga madrasa nyingi zaidi ili kuwapatia watoto mafunzo ya kiimani ambayo yatawawezesha kuwa na jamii zenye maadili.