The House of Favourite Newspapers

Rais Erdogan Atimua Mabalozi 10

0

RAIS  wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuagiza waziri wake wa mambo ya nje kuwatimua mabalozi wa nchi 10, zikiwemo Ujerumani na Marekani, walioomba kuachiliwa kwa kiongozi wa asasi za kiraia aliyefungwa jela, Osman Kavala.

 

Erdogan alisema hapo jana kuwa mabalozi hao lazima waondoke, akiwashtumu kwa utovu wa nidhamu, Siku ya Jumatatu, mabalozi hao walitoa taarifa ya pamoja isiyo ya kawaida wakisema kuendelea kuzuiliwa kwa Kavala kunaijengea mashaka Uturuki.

 

Hata hivyo, mpaka jana jioni, mataifa kadhaa ya Ulaya yalisema kuwa hayajapokea taarifa rasmi kutoka Uturuki, Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kuwa kwa sasa wako katika mazungumzo na mataifa mengine tisa yaliyotajwa kwenye amri hiyo ya Erdogan.

 

Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Norway, Trude Maseide, ameyaambia mashirika ya habari nchini humo kwamba balozi wao hajafanya lolote kuhalalisha kufukuzwa kwake.

 

Leave A Reply