The House of Favourite Newspapers

Rais Jacob Zuma Afika Mahakamani Kusikiliza Kesi Yake

Kesi ya rushwa ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anayekabiliwa na tuhuma 16 zikiwemo za udanganyifu, ufisadi na kutakatisha fedha haramu wakati akiwa madarakani, imeahirishwa hadi Juni 8, 2018, itakaposomwa tena. 

 

Zuma alifika Mahakama Kuu ya Durban leo asubuhi Aprili 6, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi yake hiyo huku wafuasi wake walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikesha kumuombea.

 

Zuma alifunguliwa mashtaka na kesi yake kusikilizwa kisha kufutwa mwaka 2009 na sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolewa madarakani na kumuachia Cyril Ramaphosa ambaye aliahidi kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi nchini humo.

JPM Azindua Ukuta wa Mirerani Manyara

Comments are closed.