The House of Favourite Newspapers

Rais JPM amteua Hebart Mrango Mwenyekiti Bodi mpya TBC

0

PIC+balozi

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Utangazaji (TBC), Balozi Hebart Mrango.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli amemteua Balozi Hebart Mrango kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika la Utangazaji TBC kuanzia February 19 mwaka huu, ambapo atakaa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Raisi amefanya uteuzi huo baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake ambayo ilikuwa ikiongozwa na Mwajabu Possi kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria.

Waziri wa Habari sanaa, Utamaduni  na Michezo Nape Nnauye ametoa wasifu wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Utangazaji TBC ilikujaza nafasi ya Mwajabu Possi ambaye amemaliza muda wake.

Aidha Waziri Nape ameteua wajumbe sita wa Bodi hiyo wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kuboresha Tasnia ya Habari, miongoni mwa wajumbe hao ni pamoja na Dk. Ayoub Rioba ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) na Asa Mwambene ambaye ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo

Baada ya uteuzi huo, Waziri Nape ameitaka Bodi hiyo kuwa wabunifu ilikuja na mbinu mbadala za kuboresha tasnia hiyo ya Habari nchini.

Hivi karibuni Waziri wa Habari Nape Nnauye alisimamisha watumishi wawili wa shirika la utangazaji kutokana na utendajii usioridhisha.

Leave A Reply