JPM: Msipokee Misaada ya Corona Hovyo, vya Dezo Vinaua – Video

RAIS  John  Magufuli amewataka wadau, taasisi, mashirika na watu wote wanaotoa misaada kwa ajili ya kujikinga na janga la corona wavikabidhi katika Wizara ya Afya ili vihakikiwe kabla ya kusambazwa na kuanza kutumika.

 

Amesisitiza kwa Wizara ya Afya kwamba pindi ikipokea vifaa na kuvipima ikagundua vina virusi vya Corona vilivyopandikizwa makusudi, wahusika wa misaada hayo wapelekwe mahakamani na kufunguliwa kesi ya jina au hata ya mauaji.

 

Amesema hayo leo Alhamisi, Mei 21, 2020, katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali ambao aliwateua hivi karibuni.

 

Pamoja na maagizo hayo pia aliwaasa viongozi aliowaapisha wakafanye kazi kwa nguvu kwa ajili ya manufaa ya Tanzania.

 

“Corona imeshuka sana… Nimetembea kwa gari kutoka Geita mpaka Dodoma, nimecheki watu njiani, hakika wanafanya kazi. Waziri wa Afya anajituma kwelikweli, katika suala la Corona, japokuwa yeye si daktari,” alisema akimsifia Waziri Ummy Mwalimu na kuongeza kwamba alikuwa anapigiwa simu zaidi ya mara nane kuhusiana na suala la Corona lakini aliisimamia  wizara hiyo kwa ujasiri mkubwa.

 

Alisisitiza kwamba wananchi waendelee  kuchukua tahadhari, kwani pamoja na kasi ya ugonjwa huo wa  COVID-19 kupungua, bado vita vya kupambana nao vinatakiwa viendelee.

 

“Niwaombe ndugu zangu Watanzania kwenye hili (la kupokea misaada) tuchukue tahadhari kubwa…  tusije kubambikiziwa Corona kwa namna yoyote.  Mtu akileta kifaa lazima kifanyiwe assessment  (uchunguzi wa kina).  Tunahitaji misaada lakini vya dezo vinaua,” alisisitiza.

 


Loading...

Toa comment