JPM: Nimekupa Pesa za Shule, Usizitoe Mahari – Video

RAIS  John  Magufuli aliye  katika ziara ya siku tatu mkoani Rukwa kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo, leo  amemkabidhi Mwalimu Dominic Mbaraka Mjema, kiasi cha Sh. milioni  tatu taslimu kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule mkoani humo.

 

“Mwalimu Mjema nimekupa hizi pesa usizitafune, nimetoa kwa ajili ya shule, usiende kuzitolea mahari, nitafuatilia,” amesema Magufuli katika mazingira ya utani.

Aidha, akizungumza na wananchi wakati akielekea Nkasi, ameahidi kutatua tatizo la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

 

“Uongozi wa Mungu ni tofauti na sisi, akitaka jua au mvua inakuwa, lakini sisi lazima tufanye kazi. Hapa hapakuwa na lami, hata babu zetu waliokufa hawajui hata rangi ya lami. Serikali inafanya kazi. Diwani amesimama kwenye lami anaeleza shida tu bila hata kushukuru.

 

“Nilitegemea mheshimiwa diwani angesema mheshimiwa rais tunakushukuru kwanza kwa lami, lakini maneno yake yote hakuna hata kimoja alichoshukuru…  Na kwenye maandiko wanasema tushukuru kwa kila jambo,” alisema rais katika hotuba yake.

 

MSIKILIZE RAIS MAGUFULI HAPA


Loading...

Toa comment