Rais Kenyatta Amaliza Ziara Yake Chato, Arejea Kenya – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili Chato mkoani Geita.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ammaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini mwake. Katika ziara yake hiyo Kenyatta, amemjulia hali mama mzazi wa Rais Dkt. John Magufuli ambaye anaendelea na matibabu nyumbani kwake Chato, Geita.

Kenyatta ameagana na mwenyeji wake, Rais Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Chato. Katika ziara hiyo, marais hao wamesisitiza kudumisha amani na uhusiano mzuri katika nchi za Jumuiya Afrika Mashariki na kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo biashara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakisikiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya wa Mwagazege ya Chato kabla ya Rais Kenyatta kuondoka na kurejea nchini Kenya.

 

 

 

TAZAMA TUKIO HAPA

Loading...

Toa comment