Rais Kenyatta Atua Chato, Amtaja Jaguar, Taifa Stars – Video

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta,  ameshawasili nchini leo Ijumaa, Julai 5, 2019 na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato mkoani Geita kwa ziara binafsi na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyeko mapumziko Chato.

 

Rais Kenyatta amesema:

Kitu nachopenda kama Rais wa Kenya ni kuona Wanaafrika Mashariki tuko pamoja, unasikia wengine wanaropoka mambo mengi ambayo hayapo, unawezaje kumwambia Mtanzania huwezi tembea Kenya, au kumzuia Mkenya kuja Tanzania kufanya biashara.

 

Nikiwa hapa siku ya leo kama Rais wa nchi jirani, nchi ndugu wa Tanzania  leo ni siku ya muhimu sana. Leo nimekanyaga hapa kwenu kama ndugu na rafiki wa Rais wenu, Magufuli. Niko hapa kwa ushirikiano mwema.

 

Tuko hapa kuimarisha urafiki na tupo na wananchi wanaojuana na wanaozungumza lugha moja ya kinyumbani na kitaifa. Ufike Namanga ni majirani kwa lugha ya nyumbani na kitaifa. Upande wa Pwani hadi Taveta ni jamii moja. Mtu anaweza kututenganisha kweli?

 

Tumarishe uhusiano wetu na kufuta vikwazo vyote hata kibiashara, watu waoane. Hakuna kitu kinaweza kuimarisha undugu kama ndoa. Na hakuna kitu mimi katika utawala wangu ningependa kuona kama East Africa inakuwa moja.

 

Nasikia kuna watu wanaropoka huko (Mbunge na Msanii Jaguar). Unawezaje kuzuia Mtanzania asifanye biashara Kenya au Mkenya asifanye Biashara Tanzania. Tunataka kushirikiana na kuona ushirikiano unakua na ndio maana tumeona sio kila siku ziara za kitaifa, leo nataka nikale Sato kwake.

 

Juzi tumepambana Cairo, Harambee Stars na Taifa Stars. Naamini hakuna mtu alilala siku ile. Lakini Harambee ikaichapa Tanzania. Na nyie mlinufaika siku ile ya Senegal sisi tulichapwa 3 nyie 2. Ila ndio tujipange ikija siku nyingine fainali ni sisi.

 

“Haiwezekani siasa tuanze nayo kila wakati ukinywa chai siasa, ukienda lunch siasa ukienda kwa mpenzi wako ni siasa haiwezekani kila siku ni siasa ina wakati, tujipange kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu. mambo hayo ndiyo yatabadilisha maisha,” amesema Rais Kenyatta.

TAZAMA TUKIO ZIMA

Loading...

Toa comment