The House of Favourite Newspapers

Rais Kenyatta, Mkewe, Wapata Chanjo ya Corona

0

Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza maafisa wakuu wa serikali kupokea chanjo ya corona katika Ikulu ya Nairobi.

 

 

Baada ya kutangaza masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya Covid 19 nchini Kenya rais alikuwa wa kwanza kuchanjwa kisha mkewe Margaret Kenyatta akachomwa chanjo hiyo.

 

 

Wengine waliochanjwa ni waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i , Waziri wa Afya Mutahi Kagwe waziri wa mashauri ya kigeni Raychelle Omamo ,Kaimu Jaji mkuu Philomena Mwilu na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kidini.

 

 

Rais amewasisitiza Wakenya wachanjwe dhidi ya virusi hivyo baada ya serikali kutangaza kwamba itawapa kipaumbele watiu walio na umri wa miaka 58 na zaidi katika kutoa chanjo hiyo .

 

Wakati huo huo, Rais Kenyatta amezifunga kaunti tano nchini Kenya kutokana na ongezeko la wagonjwa wa corona.Kaunti hizo ni Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru. Marufuku hiyo inaanza ifikapo saa sita usiku.

 

 

Hakuna usafiri wa barabarani,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kuondoka katika sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga ‘kubwa la corona’.

 

 

Maeneo hayo yatakuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 zijazo . ‘Ukiwapima Corona Wakenya 100 ,20 watapatikana na virusi hivyo.Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi’ rais Kenyatta amesema. Rais Uhuru amesema wimbi la tatu la janga ilo nchini Kenya linatarajiwa kufika kilele chake katika siku 30 zijazo.

Leave A Reply