Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi

JK Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi nchini Kenya, Mhe. Bayani V. Mangibin. Hafla hiyo imefanyika Ikulu Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2015.

JK 2

Balozi Mangibin akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

JK 3

Balozi Mangibin (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberatta Mulamula (kushoto) mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete (katikati mwenye tai nyekundu).
Toa comment