visa

Rais Kim Jong Un Kutekeleza Adhabu ya Kifo, Watu Kufanywa Kitoweo!

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un,  amefanya majaribio ya njia mpya ya adhabu ya kifo kwa kumWadhibu kiongozi mmoja wa jeshi nchini humo aliyedaiwa kupanga jaribio la kuipindua serikali yake.

 

Adhabu hiyo ya kifo kwa sasa itakuwa ni ya kutumbukizwa kwenye bwawa la samaki wakali aina ya Piranhas ili abaki kuwa kitoweo cha samaki hao.

 

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail,  adhabu imeanza kutumiwa kwa mara ya kwanza kupitia kwa kiongozi huyo wa jeshi.

 

Mabwawa hayo ya kisasa (aquariums) yamejengwa katika makazi ya rais huyo yaliyopo Ryongsong mjini Pyongyang.  Kwa mujibu wa picha zilizopigwa na kituo cha runinga cha taifa hilo, zilimwonesha mhukumiwa huyo akihangaika kwenye mabwawa hayo huku akionekana hana mikono na miguu.

 

Mpango wa adhabu hiyo mpya,  ni wazo lilitoka katika filamu ya “The spy who loved me” ambapo kwenye filamu hiyo kuna watu wanahukumiwa kwa kutumbukizwa kwenye bwawa la papa. Imeripotiwa kuwa tangu rais huyo aingie madarakani mwaka 2011, ametekeleza adhabu ya vifo kwa watu 16 wakiwemo viongozi 11 wa serikali yake.
Toa comment