The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushtukiza

0
Rais Magufuli akisindikizwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (kushoto) na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa BAKWATA unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 28, 2020

RAIS  John  Magufuli leo tarehe 28 Februari, 2020,  amekagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

…Akiwa  na viongozi  waandamizi wa BAKWATA  akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti huo. 

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.

…Akiendelea  kukagua  baadhi ya sehemu za ujenzi huo. 

Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally,  Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa msikiti huo.

…Akipita sehemu ambazo zimekamilika kujengwa.  

Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya ibada.

Mufti  amemshukuru  Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.

Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, mufti ameongoza dua ya kumuombea  Magufuli na taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.

 

…Akishiriki katika dua na  viongozi  wa  BAKWATA.

Leave A Reply