Habari JPM AZINDUA DARAJA LA ‘MAGUFULI’ KILOMBERO (Picha + Video) Last updated May 5, 2018 Share Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Wabunge wa mkoa wa Morogoro na Viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akifurahia jambo na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali mara baada ya kufungua Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula kona katika Wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli lenye urefu wa M384) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akizungumza katika msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Rais Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mang’ula Mrindoko Msangi mara baada ya kumkabidhi kiasi cha Shilingi milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule hiyo. Mwanafunzi huyo alielezea kwa ufasaha kero inayowakabili shuleni hapo. PICHA NA IKULU RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 5, 2018 amezindua Rasmi Darala la Magufuli lililopo Kilombero mkoani humo. JPM Azindua Daraja La ‘MAGUFULI’ Kilombero Daraja la Jina La ‘MAGUFULI’ Lazinduliwa Leo Darala MagufuliJohn Magufuli Share
Comments are closed.