Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam leo Januari 11,2016 Rais Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam leo.
Rais Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku.
Rais Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia
Rais Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016