RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali na maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mwasisi na Mkurugezi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, aliyefariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Magufuli leo Machi 2, 2019 aalifanya hivyo katika viwanja vya Karimjee, akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete; mawaziri, wabunge na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.
Comments are closed.