The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli amuapisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

majaliwaaWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, muda huu amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma.

Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.

Comments are closed.