The House of Favourite Newspapers

Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya CCM Dar Leo

0

KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imekutana jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho chini ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.  Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Magufuli akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, akiwasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwa kaongozana na Kinana wakiwasili katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Magufuli na wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa katika matayarisho ya mwisho kabla ya kikao.
Mwenyekiti wa CCM, Rais  Magufuli akijitayarisha kuanza kikao cha Kamati Kuu.
  Hali ilivyokuwa katika chumba cha kikao cha Kamati Kuu ya CCM.
Leave A Reply