Rais Magufuli Aongoza Mamia Kuaga Mwili wa Majuto, Dar

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiaga mwili wa marehemu Amri Athumani ‘Mzee Majuto’  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, akiaga mwili wa marehemu Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.

Rais Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali.

Rais Magufuli akiondoka katika ukumbi wa Karimjee baada ya kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Majuto.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akitoa pole kwa wafiwa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole akitoa heshima zake za mwisho.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa pole kwa wafiwa.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akitoa pole kwa wafiwa.

Muonekano wa ukumbi wa Karimjee.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amewaongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Msanii wa vichekesho nchini Amri Athuman maarufu King Majuto, katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine waliofika kumuuaga mwili wa mzee Majuto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole, Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zuberi, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar,  Alhadi Salum  na wengineo.

Mzee Majuto alifariki jana Jumatano Agosti 8, 2018 saa mbili kamili usiku katika Hospitali ya Taifa ya  Muhimbili jijini Dar es Salaam na mwili wake kusafirishwa kwenda Tanga mjini ambako mazishi yatafanyika kesho.

(PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL)

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment