Rais Magufuli atangaza baraza lake la mawaziri

BREAKINGNEWS3

jbb1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015.
Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.jbb2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri.

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora

Mawaziri – George Simbachawene  na Angela Kairuki

Naibu Waziri – Sumeilam Said Jaffo

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri – January Makamba

Naibu Waziri – Luhaga Joelson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Jenista Muhagama

MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri – Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri – William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri Bado hajapatikana

Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri Bado hajapatikana

Naibu Waziri – Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini

Waziri – Prof. Mwijarubi Muhongo

Naibu Waziri – Medard Kalemani

Wizara ya Katiba na Sheria,

Waziri – Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

Waziri – Dk. Augustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri – Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri – Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri – William Lukuvi

Naibu Waziri – Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri Bado hajapatikana

Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri Charles Mwijage

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi

Waziri Bado hajapatikana

Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Ummy Mwalim

Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangalla

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri – Nape Nnauye

Naibu Waziri – Anastasia Wambura

Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri – Prof. Makame Mbarawa

Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

MAFGUFULI (2)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais, Waziri Mkuu na katibu mkuu kiongozi wakiwasili moja ya kumbi za mikutano ya ikulu kwa ajili ya Rais kutangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 10,2015.MAFGUFULI (1)MAFGUFULI (6)MAFGUFULI (10)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana kwa furaha na wanahabari mara baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 10, 2015.MAFGUFULI (3)MAFGUFULI (4)MAFGUFULI (7)MAFGUFULI (8)Picha ya pamoja na Waandishi wa habari baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Desemba10,2015MAFGUFULI (9)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akirejea ofisini baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Swali: Kuna baadhi hukutaja, tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma ukiondoa TAMISEMI?
Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata. Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.

Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?

Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.

Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?

Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.

Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.

Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.

Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharejesha zile hela?

Magufuli: Swali hilo kamuulize kamishna wa kodi TRA.

SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?

Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.

Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?

Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.

Asanteni sana na ninawashukuru

Loading...

Toa comment