RAIS MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 4,477 – VIDEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Magufuli ametoa salamu za Kumbukumbu ya Miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, leo Ijumaa, Desemba 7, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Akituma salam hizo, Rais Magufuli kwa mujibu wa Ibara ya 45 Ibara ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza msamaha kwa wafungwa 4,477 waliyokuwa wamefungwa / kuhukumiwa kwenye magereza mbalimbali nchini ambapo  kati yao 1,176 wataachiwa Desemba 9, 2018 katika Sikukuu ya Uhuru.

 

“Msamaha huu utawahusu wafungwa ambao ni wagonjwa, wazee kuanzia miaka 70 na zaidi, wafungwa wa kike walioingiia gerezani wakiwa wajawazito au na watoto, wanaonyonya na wasionyinya, wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili. Nimeamua wafungwa wote waliotumikia robo za adhabu zao wapunguziwe robo baada ya punguzo la kawaida la theluthi moja kwa mujibu wa sheria.

 

“Msamaha hautawahusu Wafungwa wanaotumikia baadhi ya adhabu zikiwemo Kunyongwa, Kifungo cha maisha, biashara ya Dawa za kulevya, biashara za Binadamu, kukutwa na viungo vya Binadamu, Walionajisi na waliowapa mimba Wanafunzi,” amesema Magufuli.

 

“Ninawatakia Watanzania wote kila la heri katika Maadhimisho ya Miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, tusheherekee kwa amani, Mungu wabariki Watanzania wote, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.” amesema Rais Magufuli.

 

Aidha, Magufuli amesisitiza kuwa fedha iliyotengwa kwa ajili ya sherehe za Uhuru Desemba 9 mwaka huu, kiasi cha Tsh. Bilioni 1, itatumika kujenga Hospitali mpya ya Uhuru jijini Dodoma.

BREAKING: RAIS MAGUFULI Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 4477

Toa comment