Rais Magufuli Ateua Viongozi TTCL, Airtel

RAIS  John Magufuli amemteua Mohammed Abdallah Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

 

Mtonga anachukua nafasi ya Dkt. Omari Rashid Nundu ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

 

Uteuzi wake unafuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania anapaswa kuteuliwa na Serikali ya Tanzania.

 

Kwa mujibu wa makubaliano hayo Ofisa Mkuu wa Ufundi (Chief Technical Officer – CTO) pia anateuliwa na serikali  na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt. Prosper Godfrey Mafole.

 

Wajumbe wengine watakaoiwakilisha Serikali katika Bodi ya Airtel Tanzania ni John Marato Sausi na Lekinyi Ngariapusi Mollel.

 

Uteuzi huu unaanza leo June 12, 2019.

Loading...

Toa comment