The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Rais Magufuli Atoa Onyo Kali kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amevikosoa vyombo vya habari nchini Tanzania na kuwataka wamiliki wa vyombo hivyo kuwa makini kama wanadhani wana uhuru wa namna hiyo.

“Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari nchini muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna, basi kuweni makini sana.”

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha mabalozi, Mawaziri wateule pamoja na Katibu Mkuu wa Ikulu.

Miongoni mwa viongozi hao waliokula kiapo leo kutimiza majukumu yao ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison George Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Ikulu, Alphayo Kidata.

Akizungumza baada ya viongozi hao baada kula kiapo, Rais Magufuli amewasihi waandishi wa habari kuwa wazalendo huku akisema kuwa ikifika mahali Tanzania inaharibika, wao pamoja na wanaowatuma juu ya nini cha kuandika pia wataharibikiwa.

Aidha, amevikosoa baadhi ya vyombo vya habari kwa kusema kuwa, vimekua vikitoa muda mwingi zaidi kuhusu sehemu zenye migogoro kuliko kuandika habari za maendeleo

“Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, ‘watch out.’

“Hata magazeti ya leo ukiyaangalia, yana picha ya mtu mmoja ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kosa hilo linaungwa mkono na serikali.”

Akitolea mfano ujio wa Rais wa Benki ya Dunia nchini, Rais Magufuli alisema kuwa siku iliyofuatia vyombo vya habari vingi havikuelezea tukio lilitokea pale Ubungo lakini viliandika habari nyingine tofauti.

“Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi”, alisema Rais Magufuli.

Lakini pia alikosoa taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari ikidai kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana angezungumza na waandishi wa habari leo wakati yeye amemtuma nchini India ambapo atakuwa huko kwa muda wa zaidi ya siku 10.

Namshukuru Waziri Dkt Mwakyembe amekuja hapa kuapa sababu jana kwenye mitandao kuna wengine walikuwa wakisema hatokuja kuapa, na nilikuwa nasubiri nione” alisema Rais Magufuli

==>Tazama hii Video kumsikiliza Rais Magufuli akiongea Pamoja na walichoongea wateule wa Rais

Comments are closed.