Rais Magufuli Awaapisha Mabalozi Wanne – Video

 

RAIS  John  Magufuli, leo Jumanne, Januari 14, 2020, amewaapisha mabalozi wanne  watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na Nigeria.


Walioapishwa ni Mej. Jen. Mstaafu Gaudence Salim Milanzi anayekuwa Balozi wa Tanzania Pretoria – Afrika Kusini;  Dkt. Modestus Francis Kipilimba (Windhoek – Namibia);  Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah (Harare – Zimbabwe) na Dkt. Benson Alfred Bana (Abuja – Nigeria).


Baada ya kuwaapisha,  amewataka kuripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya wiki mbili  kuanzia sasa na amewasisitiza kwenda kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia maslahi ya taifa hasa kiuchumi na kuwawezesha Watanzania kupata ajira katika fursa zilizopo katika nchi hizo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka mabalozi hao kufuatilia maeneo yote ambayo rais  alikubaliana na marais wenzake alipotembelea nchi hizo hivi karibuni, na pia kuitangaza vyema Tanzania ambayo kwa sasa inapiga hatua kubwa katika maeneo mengi.


Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam,  na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Samia  Hassan na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa.


Loading...

Toa comment