The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI SIMBA KOMBE LA UBINGWA WA VPL 2017-18

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli akijiandaa kumkabidhi kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu nahodha wa Simba, John Bocco.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana amewakabidhi Klabu ya Simba kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar baada ya kumalizaka kwa mchezo kati ya timu hiyo dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wa Simba wakishangilia ubingwa wao baada ya kukabidhiwa kombe.

Mchezo huo ambao uliisha kwa Simba kuchapwa bao 1-0 na kuzima ndoto ya kumaliza ligi bila kufungwa.

Rais Magufuli hakuvutiwa na kiwango walichoonyesha Simba jana dhidi ya Kagera na kuongeza kuwa wakiendelea kucheza hivyo hawataweza kuchukua kombe la ubingwa wa Afrika hivyo amewataka wajipange ili waweze kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Nderemo zikiendelea kwa wachezaji wa Simba baada ya kukabidhiwa kombe lao.

Aidha Rais Magufuli amewaomba viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wale wa klabu kuweka mikakati ya ushindi kwa timu za Tanzania kwani amechoka kuona zikishindwa kufanya vizuri kimataifa.

Ofisa Habari wa Simba, Hajji Manara akishangilia pamoja na viongozi na wachezaji wa timu hiyo.

Wakati huohuo, Kocha wa Simba, Pierre Leichantre amewapongeza wachezaji wake kwa kutwaa ubingwa na kuwapa raha mashabiki wao.

Mlinzi wa Simba, Erasto Nyoni na wachezaji wenzake wakiwa wamembeba kocha wa timu hiyo, Pierre Leichantre baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa.

 

“Niseme wazi kabisa mimi ni shabiki wa Taifa Stars, huwa nafuatilia mpira wa ligi za ndani na nje, hadi Jumamosi wiki iliyopita timu mbili tu zilikuwa hazijafungwa mpaka zinachukua ubingwa Barcelona ya Hispania na Simba.

 

”Tangu uongozi mpya wa TFF umeingia madarakani unajitahidi kuonesha jitihada katika kuendeleza mchezo huu, niviombe vyama vingine vya michezo viige mfano huo. Nimefurahi mchezo wa leo ulikuwa umetulia, nina uhakika leo tutaondoka na kuacha viti vikiwa salama uwanjani. Mh. Waziri ukinialika tena nitakuja.

 

“Niwaombe Simba muwe wa kwanza kulileta Kombe la Afrika hapa, ila kwa kiwango mlichocheza leo hamuwezi kushinda kombe hilo. Nimepigiwa kura na wanamichezo, nimepigiwa kura na Yanga, nimepigiwa kura na Simba. Nitumie fursa hii kukiomba Chama Changu cha CCM ambacho kinamiliki viwanja kwa asilimia kubwa viboreshe viwanja hivyo

 

“Tutashirikiana na TFF kupitia Wizara ya Habari kuiandaa timu ya vijana (Serengeti Boys) ili mwakani iubakize hapa ubingwa wa Afrika na kuondoa zana ya Kichwa cha Mwendawazimu,” amesema Rais Magufuli.

PICHA: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.