Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi

magufulika (1)Hapa kazi tu ya  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph
Magufuli  ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais  huyo aonekanavyo pichani akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli,wakishiriki kufanya usafi leo ndani na nje viunga vya Ikulu ikiwemo pia soko la Samaki Feri,ambako alipata wasaa kuwasikiliza wachuuzi wa samaki na wavuvi.

magufulika (2)
magufulika (3)Rais Magufuli akiokota taka taka katika eneo la ufukwe wa ferry akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli jijini Dar es Salaam.
magufulika (4)
magufulika (5)
magufulika (6)
magufuliiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akishirikiana na wananchi wengine kufanya usafi.magufuliRais Magufuli na mkewe, Mama Janeth Magufuli  wakiwa na baadhi ya wananchi wakifanya usafi.
Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameongoza Watanzania kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi, yuko eneo la ufukwe karibia na Ikulu akifanya usafi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye yuko kwenye soko la Kariakoo akiongoza wafanyabiashara wa soko hilo kufanya usafi.
Ni siku ya kihistoria kwa taifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwamba siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania watu huelekea viwanja vya Uhuru kuungana na wengine kuadhimisha siku hii ambapo leo ni miaka 54 tangu uhuru kupatikana,lakini  watu wanafanya usafi kuboresha mazingira ikielezwa ni UHURU na KAZI,ikienda sambamba na kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu.
Loading...

Toa comment