The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Awapa Serengeti Boys Bilioni 1 – Video

Rais Johh Magufuli atoa zawadi ya viwanja vya kujenga nyumba kwa wachezaji wa taifa stars pamoja na bondia Hassan mwakinyo baada yakuipa Tanzania ushindi pamoja na fedha taslimi shiling bilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya AFCON kwa timu ya vijana chini ya miaka 17.

 

“Tangu Taifa Stars ilipofungwa na Lesotho, na TZS milioni 50 zangu wamekula iliniuma kweli kweli. Sikuwahi kuongea na Dk Mwakyembe tangu siku ile hadi leo asubuhi nilipompigia. Aliniandikia meseji kuwa tuwe na Kombe la Magufuli, kama ilivyo Kagame Cup, sikumjibu.

 

“Inaumiza sana kwa nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya Milioni 55 kufungwa na nchi yenye watu Milioni moja, ni lazima tujiulize ni kweli kwa nchi yenye watu Milioni 55, tunakosa wachezaji 11 tu wenye vipaji kuiwakilisha nchi?

 

“Raha niliyoipata jana na ahadi ya kwamba tukishinda tunaenda Kombe la Dunia, tukubaliane nikimwaga hela hapa na nyie mkamwage magoli, najua imetolewa fedha na sisi kama Taifa lazima tutoe fedha, tutatoa Tsh. Bilioni 1, angalau zisaidie maandalizi haya.

 

“Rais Magufuli amesema serikali itatoa Tsh. Shilingi 1b, kwa ajili ya kuiwezesha Serengeti Boys kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa Miaka 17, AfconU17 yatakayofanyika nchini Tanzania mwezi Aprili mwaka huu.

TAZAMA TUKIO HILO

Comments are closed.