The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kutumbua Watumishi 9,932 Dodoma, Rais Magufuli Aibukia Kilimanjaro

0

KILIMANJARO:  Rais John Pombe Magufuli leo Aprili 29, 2017 amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo atafanya ziara ya kikazi kwa muda wa siku tatu.

Sambamba na ziara hiyo, Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambapo atakuwa mgeni rasmi.

Rais amewasili nchini mkoani humo ikiwa ni siku moja baada kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma ambapo watumishi 9,932 aliwatimua kazi baada ya kubainika kuwa wamegushi vyeti.

 

Kimenuka, Magufuli Akabidhiwa Majina ya Watumishi Wenze Vyeti Feki, Awatimua Kazi 9,932

Leave A Reply