JPM Azindua Safari za Ndege Dar-Mpanda (Picha +Video)

Rais John Magufuli akiwa na mkewe,  Janeth Magufuli, ma viongozi wa Mkoa wa Katavi, wabunge, mawaziri na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)  kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo 12/10/2019.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli  leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 amezindua safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi.

Amesema hadi leo Jumamosi watu 138 waliokuwa wakidaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuomba msamaha kwa DPP, wamerudisha fedha, wametubu na kuachiwa.

Aidha,ameongeza kwamba:

“Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao. Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.”

Amesema kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha na wataendelea kuachiwa kadri watakavyorudisha fedha na fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo

Rais Magufuli akiondoka kuelekea mkoani Dodoma  kutumia usafiri wa shirika la ndege la ATCL baada ya uzinduzi huo.

…Akiwashukuru wananchi wa Mpanda, Katavi,  akielekea mkoani Dodoma.


Loading...

Toa comment