RAIS MAGUFULI, KUHITIMISHA KILELE CHA MWENGE ZANZIBAR

Rais Magufuli Alipowasili Leo Katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, anatarajia kuhitimisha kilele cha Mwenge, kisiwani Zanzibar katika mkoa wa mjini Magharibi, mnamo Oktoba 14, mwaka huu, ambapo pia itakuwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud

 

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud, amesema kuwa, Wazanzibar wamefurahi sana kuona kwa mara ya kwanza kilele cha Mwenge kinahitimishwa kisiwani kwao.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Akiwa Ameushika Mwenge wa Uhuru

“Zanzibar itaweka historia kubwa kwa mara ya kwanza kuwakutanisha viongozi wakubwa wa nchi katika kilele cha Mwenge, akiwemo rais wa Tanzania, Dkt John Magufuli, rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu mkuu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa rais Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddy.” RC Ayoub

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment