The House of Favourite Newspapers

JPM: Sijatuma Mtu, Wapimeni Wenyewe – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekanusha taarifa za baadhi ya watia nia wa ubunge na nyadhifa nyingine ambao wamekuwa wakipita kuwahadaa wananchi na viongozi wa vyama kuwa amewatuma yeye kwenda kugombea katika maeneo hayo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

 

Magufuli amesema hayo leo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliyowaapisha leo, Julai 16, 2020.

 

“Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais, waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000, mpaka leo asubuhi wagombea kupitia CCM ni; Dar 829, Arusha, 320, Kusini Unguja 53, Kilimanjaro 82, Kagera 328, jumla watia nia kwenye majimbo ni 6533, viti maalum 1539 na wawakilishi 133, jumla kuu 8205. Bado kuna leo na kesho, hii inadhirishia CCM watu wanakipenda.

 

”Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982. Mwanadamu unapoishi lazima utosheke na kile ulichonacho sasa unapokuwa unahaha huku na huku sijui Mungu atakufungulia njia ipi lakini niwaombe viongozi mliapishwa leo mkasimame katika majukumu yenu, fanyeni kazi na kutumikia wananchi.

“Nawapongeza wote waliochukua fomu kugombea kupitia CCM, lakini nimesikia kila mahali ‘mimi nimetumwa na Rais’ kama nina uwezo wa kutuma kwa nini nihangaike kukutuma, si ningesubiri kwenye viti vyangu kumi nikakuteua kama nitashinda, kwa hiyo sikutuma mtu, nataka Watanzania muelewe, nataka muwatume ninyi.

 

“Nataka kuwathibitishia wananchi wote, hakuna mtu yeyote aliyeumwa na mimi, wala Makamu wa Rais, wala Waziri Mkuu, wala mzee Mangula wala Katibu Mkuu wa CCM. Wanaosema nimewatuma ni waongo, wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanawafaa. Siwezi kutuma mtu kwa mgongo wa pembeni.

“Dkt Luhende wewe umekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hata wewe Kanali Songea tumekupeleka Kiteto migogoro ipo mingi pale tumekupeleka ukashughulikie hilo, wakiona nyota hizo wataogopaaa nyingine.

 

“Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Mmefanikiwa kuipata fursa, hivyo makafanye kazi, amesema Rais Magufuli.

 

Leave A Reply