Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awasili na Kuingia Kwenye Treni – Picha
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameshawasili na kuingia kwenye treni hapa Stesheni ya treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) Dar es Salaam.
Hii ni treni ya kwanza ambayo itatangulia na kisha baadae itafuata ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Ni uzinduzi wa treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR), ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anasafiri kwa treni kuanzia Dar es Salaam mpaka Dodoma.