Rais Mstaafu Kikwete na Mkewe Wafika nyumbani kwa Hayati Ali Hassan Mwinyi kutoa pole kwa familia-Video

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na mkewe ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete leo Machi 1, 2024 wamefika nyumbani kwa Rais Mstaafu, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Mikocheni mkoani Dar es Salaam kutoa pole kwa familia kufuatia kifo cha kiongozi huyo.