Rais Mwinyi Afika Banda la Tigo Kujionea Teknolojia Mpya Katika Mtandao Huo
Katika kuhitimisha maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara Kampuni ya Mtandao wa simu ya Tigo Tanzania imepata ugeni wa heshima katika banda lao baada ya kutembelewa na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ambapo amejionea huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo.
Dr.Mwinyi ameipongeza Tigo kwa juhudi zake na kufikisha huduma kwa jamii hasa wenye kipato cha chini kwa kuwafungulia dunia kupitia mawasiliano.
Kampuni hiyo imeleta simu za mkopo ya 4G aina ya ZTE A34 Blade kwa kianzio cha sh 35000 tu na malipo 650 kila siku kwa muda wa mwaka mzima ili huduma ya mawasilino iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi hapa nchini.