The House of Favourite Newspapers

Rais Dkt. Hussein Mwinyi Atembelea Kijiji Cha Bima

Mamlaka ya usimamizi wa bima nchini (TIRA) imesema sekta ya bima inakuwa kwa wastani wa asilimia 15 ambapo takwimu za mwaka 2023 zinaonesha ongezeko la watumiaji wa bima walifikia milioni 12 ikilinganishwa na watumiaji wa huduma za bima milioni 6 kwa mwaka 2022.

Yamesemwa hayo mara baada ya Raisi wa Seriakali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kutembelea kijiji cha Bima katika Maonesho ya 48 ya Kimatiafa ya Biashara maarufu (sabasaba) ambayo yamefikia ukomo hii leo julai 13,2024.

Akizungunza jijini Dar es salaam kamishna wa bima kutoka Mamlaka ya usimamizi wa bima nchini, Baghayo Saqware amesema Bima za mali ndizo zinazo ongoza kwa asilimia 12 ikilinganishwa na bima za maisha ambazo idadi ya watumiaji bado ni kidogo akiweka bayana kuwa elimu zaidi inahitajika kutolewa ili watanzania watumie huduma za bima ya maisha kutokana na manufaa yake kuwa ni makubwa .

Kupitia maonesho hayo ya sababa kamishna amesema  yamekuwa na tija katika kutoa elimu ya bima ambapo zaidi ya watu 5000 wamefikiwa na elimu ya bima kutoka katika kampuni 40 zilizokuwa zikitoa huduma za bima katika maonesho ya sabasaba kupitia kijiji cha bima

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Bima, Agustino ndabaha amesema miongoni mwa waliofikiwa na elimu ya bima ni pamoja na wanafunzi ambao ndio watumiaji wa huduma za bima miaka ijayo.

Takwimu zinaonesha kuwa kwa sasa sekta ya bima inachangia katika pato la Taifa kwa asilimia 1.99 kwa takwimu za mwaka 2023 huku matarajio ikiwa ni kuwezesesha sekta ya bima kuchangia kwa asilimia 3 katika pato la taifa ifikapo mwaka 2030.